Thursday, October 27, 2011

HEKA HEKA MBAGALA WAKATI FATAKI ZA SHEREHE ZA DIWALI ZIKIAMBATANA NA MILIPUKO YA FATAKI NA FASHIFASHI JIJINI DAR

LEO NI DIWALI, SIKUKUU YA WAHINDU INAYOSHEREHEKEWA MWANZO AMA MWISHO WA MWAKA KILA MWAKA. LAKINI KWA NDUGU ZETU WANAOISHI MAOLENEO YA MBAGALA, HUSUSAN KARIBU NA KAMBI YA JESHI, IMEKUWA KERO NA TISHIO KWA MAISHA YAO.

BAADA YA FATAKI NA FASHIFASHI KUANZA KURUSHWA ENEO HILO, WAKAAZI WENGI WAMEKIMBIA MAKAZI YAO WAKIJUA KWAMBA NI YALE YALEEEE...YAANI MABOMU YAMEANZA KULIPUKA TENA. UJUMBE KIBAO WA SMS UMEIFIKIA GLOBU YA JAMII KUELEZEA WAHAKA HUO NA KUBAINISHA KUWA UKWELI SIO MABOMU YA KIJESHI BALI NI SIKUKUU YA NDUGU ZETU WA-HINDU MAARUFU KAMA DIWALI.

UJUMBE HUO UNASEMA CHA KUSHANGAZA NI KWA NINI ISINGETOLEWA MAPEMA TAARIFA KUWA KUNA MILIPUKO LEO?? NA KWAMBA HUKO MBAGALA WATU WANAKIMBIZANA OVYO, WAKIASHA FAMILIA ZAO HUKU VIBAKA WAKIJISEVIA BILA UPINZANI WOWOTE.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments: