Wednesday, October 26, 2011

Picha Mbalimbali Za Ajali Mbaya ya Basi Maeneo Ya Misugusugu Kibaha Mkoani Pwani

Mkuu wa Mokoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akizungumza alipofika eneo la tukio.
Moja ya maiti ambazo ziliteketea kwa moto kufuatia ajali ya basi la Delux Coach lilopata ajali ya kupasuka gurudumu la mbele maeneo ya Misugusugu Wilayni Kibaha mkoani Pwani Oktoba 25,2011na kupinduka kabla ya kuwaka moto na kupoteza maisha ya abiria wa basi hilo takribani 25 na wengine zaidi ya 17 kujeruhiwa vibaya. Basi hilo lilikuwa linatokea jijini Dar es Salaam likielekea Dodoma.
Maiti zilikuwa ni nyingi na hata utambuzi wake ulikuwa mgumu.
Wananchi na polisi wakiangalia mabaki ya basi hilo baada ya kuteketea kabisa kwa moto.
Mmoja wa watu waliokuwa wakitoa mabaki ya miili ya watu walioteketea kwa moto akiendelea na zoezi la kuangalia iwapo kama kuna masalia yeyote.
Basi liliteketeakabisa na mabaki ya miili ya watu ililazimu kukusanywa kwa beleshi.Picha zote na Yassin Nicas Mtei



No comments: