Sunday, October 16, 2011

Miss Tanzania 2011 Aasili (Adopt) Mtoto


Miss Tanzania 2011 Salha Esrael wakishirikiana na kipindi cha Njia
Panda jioni ya leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo
pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa
watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja katika hospitali ya Taifa
Muhimbili kwenye Wodi ya Watoto namba 36 (Neonatal Ward).Pichani Miss
Tanzania 2011,Salha Esrael akiwakabidhi baadhi ya vitu Manesi wa wodi
hiyo maalum ya watoto kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akikabidhi pampas kwa ajili ya wodi
hiyo maalum kwa watoto wnaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi
mmoja,watoto hao ambao wamekuwa wakizaliwa hivyo kutokana na kukumbwa
na matatizo mbalimbali.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akimtazama mtoto wake ambaye
ameamua"kumuadapti" na kumpachika jina lake la Salha.
Mlimbwende huyo,Salha kwa hivi sasa ameamua kujikita kwenye harakati
za kutetea haki za watoto wachanga walio chini ya umri wa mwezi mmoja
ambao kitaalamu wanaitwa Neonates, "watoto hawa wamekuwa wakisahauliwa
kwa kiasi kikubwa,watu wanawakumbuka kuwasaidia watoto kuanzia miaka
mitano na kuendelea,wanakimbilia kutoa vyandalua na mambo
mengine,lakini ukweli ni kwamba kundi la watoto hawa limesahaulika
mno,kwa hiyo kupitia Miss Tanzania 2011 tukishirikiana na kipindi cha
Njia Panda tumetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za
maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto hawa
ambao wamekuwa wakisahaulika siku hadi siku",alisema Salha.
Aidha Miss Tanzania 2011 Salha Esrael “amemuadapti” mtoto ambaye ni
yatima mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja na kumpa jina la
Salha,mtoto huyo ambaye kwa sasa anaonakana kuendelea vyema kiafya
alikutwa ametupwa vichakani na kuokotwa na wasamaria wema ambao
walimfikisha haraka kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wodi ya
watoto namba 36 (Neonatal Ward).Miss Tanzania 2011 Salha amebainisha
wazi kuwa atahakikisha anamlea mtoto huyo katika maisha yake yote.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kuvikabidhi vifaa hivyo mapema
leo jioni kwa manesi wa wodi hiyo,Salha alisema kuwa yeye atajikita
zaidi katika kutetea haki za watoto hao wachanga ambao wamekuwa
wakisahaulika kwa asilimia kubwa,ilhali watoto wengi wanaanzia kwenye
hatua hiyo, “huu ni mwanzo tu wa kampeni hii,lakini nitakaporudi
kwenye mashindano ya Miss Word yanayotarajiwa kufanyika hapo baadaye
mwaka huu,mimi pamoja na wadau wengine tutahakikisha tunafanya kampeni
kubwa ya kuihamasisha na kuielimisha jamii katika suala zima la
kuwasaidia watoto hawa,ambao baadhi yao hutelekezwa na wazazi wao
kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali wangali wachanga”,
Salha akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima aliyezaliwa chini ya umri
wa mwezi mmoja na Mama yake kufariki na kuhifadhiwa kwenye chumba
maalum cha kuhifadhia watoto hao.
na Ahmad Michuzi

No comments: