Monday, October 17, 2011

Mkutano wa 125 wa Chama cha Muungano wa Mabunge Ulimwenguni waendelea nchini ujerumani

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda yuko nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa 125 wa Chama cha Muungano wa Mabunge Ulimwenguni (Interparlimentary Union-IPU). Hapa akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Uswisi Balozi A. Ngemera mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano jana jioni.
Balozi Ngemera akimpa Mhe. Spika Anne Makinda muhtasari wa mkutano
Katibu Mkuu wa Chama cha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association-CPA) Dkt William Shija akimkaribisha mkutanoni na Spika Anne Makinda.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 125 wa IPU katika mji wa Bern. Hotuba yake iliyowavuta wengi ilihusu changamoto zinazoikabili dunia ya leo: “siyo upungufu wa bajeti bali ni upungufu wa imani kwa serikali na taasisi mbalimbali”.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Abdirahin Abdi
MHE. David Kafulila akiwa na mbunge rafiki yake kutoka Canada

Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge Mhe. Hamad Rashid na aliyekuwa Mbunge wa Busega Dkt. Chegeni
Muwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel na katibu wa msafara Bw. James Warburg.
Mtoto akitoa burudani kwenye ufunguzi wa mkutano huo
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiongea na Balozi Ngemera
Spika wa Bunge Mh. Makinda na Balozi Ngemera na ujumbe wa Tanzania
wakiingia ukumbini.
Mh. Spika Anne Makinda na Spika wa Bunge la Uganga Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga wakiifuatilia hotuba hiyo kwa umakini mkubwa.
Maspika, Wabunge, Makatibu wa Bunge, Maafisa na watendaji mbalimbali katika mabunge duniani wakifuatilia hotuba za ufunguzi: Dkt. Williama Shija.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akipanda jukwaani tayari kwa kutoa hotuba yake.
Ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania: Mhe. Susan Lyimo, Dkt Chegeni (mbunge wa zamani), Mhe. Hamad Rashid na Angela Kairuki.
Picha ya pamoja ya Spika wa Bunge, Balozi Ngemera na ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania
Sehemu ya washiriki

No comments: