Monday, October 17, 2011

Waziri Mkuu Pinda Atembelea Mabanda Ya Maonyesho Mpanda

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alipotembelea banda la Mkoa wa Rukwa katka maonyesho ya uwekezaji yanayoendelea hapa wilayani Mpanda mkoa wa katavi. Maonyesho hayo ni maalum kwa ajili ya kutangaza kanda ya magharibi(Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma) katika sekta ya uwekezaji. Aliye ambatana nae(kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Rajabu Rutengwe

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisikiliza maelezo kutoa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh. Rajabu Rutengwe walipotembelea mabanda ya maonyesho ya uwekezaji yanayoendelea wilayani Mpanda, wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Stella Manyanya(MB).
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo katika banda la maonyesho la kampuni ya Katavi and kapufi ainayojishughulisha na uchimbaji na ununuzi wa madini ya dhahabu katika mikoa hiyo ya ziwa Tanganyika
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya uwekezaji yanayo fanyika wilayani Mpanda leo, pichani kulia ni mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Stella Manyanya (MB).
Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika banda la maonyesho la mkoa wa Rukwa.

Picha zote: Humphrey Alex wa Mjengwablog.com

No comments: