Wednesday, October 12, 2011

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuisaidia TAKUKURU

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akizungumzia mambo muhimu ya kisheria na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) ofisini kwake leo asubuhi. Miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza ni haki iwe inapatikana kwa wote na kwa wakati pamoja na suala zima la uzalendo kwa watendaji wote wa Serikali na mahakama.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) ameiomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa Naibu Mwanasheria Mkuu Mhe. George Masaju kuisaidia Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ya ilivyo hivi sasa.

Alimueleza hayo alipomtembelea ofisini kwake leo asubuhi ambapo atakuwa na Ziara ya siku mbili kutembelea Idara ya Mahakama, Jeshi la Magereza, Polisi na TAKUKURU.
Alimueleza kuwa TAKUKURU inatakiwa kiwe chombo makini kinachofanya mambo kwa usahihi na kwa kutoa mamaamuzi mazito na yenye uhakika zaidi.

Alimueleza kuwa elimu ikitumika vizuri ni muhimu kuweza kuepusha migogoro na matatizo ya Rushwa na haki za kibinadamu nchini. Kwa upande wake Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali alikiri na kusema kuwa nilishawaeleza TAKUKURU kuwa kwenye upande wa uelimishaji wa Umma juu ya athari na matukio ya Rushwa hawajaufanya vizuri.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimuahidi Naibu Mwanasheria Mkuu huyo kutumia ziara zake mkoani kuelimisha wananchi juu ya madhara ya rushwa, utambuzi wa haki zao za msingi, uzalendo na udumishaji wa amani ambayo ndio ngao kuu watanzania waliyojijengea kwa miaka mingi iliyopita.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili akitokea Songea ambapo atatembelea Idara ya Mahakama, Jeshi la Polisi, Magereza na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Ziara hiyo inahusu "Nationa Criminal Justice Forum" inayolenga katika kuzungumzia na kutatua matatizo yanayopatikana katika Idara ya Mahakama, Jeshi la Polisi, Magereza na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa.

Kwa mujibu wa Naibu Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali alisema kuwa katika ziara yake hiyo na kwa maeneo anayotembelea wanaweka mkazo zaidi kwenye mambo matatu muhimu ambayo ni ubora wa huduma zinazotolewa, Utambuzi na utayari katika kusimamia haki (Sensitivity to Justice) na kutilia mkazo kwenye Uzalendo katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

No comments: