Wednesday, October 19, 2011

MOTO WATEKETEZA MADUKA MANNE YA WAFANYABIASHRA ENEO LA MTAA WA SOKO MJINI SINGIDA NA KUSABABISHA HASARA YA MAMILIONI YA FEDHA.




Moto Mkubwa ukiteketeza mali pamoja na nyumba eneo la Mtaa wa soko kuu Manispaa ya Singida leo jioni.




Moto ukiendelea kuteketeza mali kwenye nyumba yenye maduka manne ya nguo, viatu simu pamoja na radio eneo la soko kuu Mjini Singida huku askari wa kikosi cha zimamoto wakisaidia kuuzima moto huo bila mafanikio.




Wananchi wakisaidia wafanyabiashara kuokoa mali mbalimbali zikiwemo masofa, na nguo eneo hilo.




Gari la zimamoto likiwa kazini eneo la tukio hilo.




Wananchi wakipakia mali kwenye gari na kuhamisha katika eneo la ajali ya moto.




Askari kanzu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mrope mwenye tisheti nyekundu akisaidia wananchi kutoa mali.


Na.Hillary Shoo.


Singida.


Moto mkubwa umezuka kwenye maduka manne ya wafanyabiashara katika mtaa wa soko kuu mjini singida na kuteketeza mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi jioni hii.


Moto huop ambao ulianza majira ya saa 9:30 alasiri hivi ulianza taratibu lakini kutokana na mji huo kuwa na upepeo mkali moto uliendelea kuwa mkubwa na kusababbisha kushika mali kwenye mojawapo ya duka mtaani hapo.


Mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio muda mfupi tangu kuanza kwa moto huo na kushuhudia maduka hayo yakishika moto mkubwa ambao hata hivyo wananchi walishindwa kuuzima.


Aidha moto huo uliendelea kushika maduka mengine ya jirani huku wananchi wakiendelea kuhamisha mali za thamani zikiwemo masofa, nguo, makabati, viatu, saa, radio pamoja na simu za mkononi.


Akizngumza eneo la tukio Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Soko, Agusti Olomi alisema moto huo ulianzia kwenye moja ya chumba cha kuoneshea video jirani na maduka hayo kutokana na hitilafu ya umeme.


Hata hivyo gari la zimamoto la Halmashauri ya Manispaa ya Singida lilifika eneo la tukio baada ya nusu saa na kukuta moto huo umesambaa kila mahali.


Lakini jambao la kushangaza ni kwamba gari hilo lilikuwa na maji kidogo hali iliyosababisha zoezi la kuzima moto huku kuwa gumu kutokana na ukosefu wa maji.


Aidha gari hilo liliondoka eneo hilo na kwenda kucghota maji mengine lakini liliporudi lilikuta mali zote zimeteketea kutokana na moto kuwa mkubwa.


Akizungumza eneo la tukio Kamanda wa polisi Mkoani Singida Celina Kaluba aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonesha katika hali ya utulivu na kufanikiwa kutoa vitu kwenye maduka ya jirani na eneo la tukio.


Aidha Kaluba amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo na thamani halisi ya mali bado haijajulikana.


Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mmoja wa wamiliki wa duka mojawapo lililoteketea aliyejtambulika kwa jina moja la Malya akizimia mara baada ya kufika katika eneo hilo na kukuta duka lake likiteketea kwa moto.


Wasamaria wema walimchukua na kumkimbiza katika hospitali ya mkoa wa Singida na kulazwa ambapao hadi tunakwenda mitamboni alikuwa nbado hajazinduka.
Habari na picha kwa Hisani ya Mo-Blog

No comments: