Friday, October 7, 2011

Mwenye Nyumba Achachamaa na Kutimua Wapangaji wote Mitaa ya Kariakoo jana

Haya ndio Maandishi yaonekanayo kwenye kuta ya nyumba hiyo iliopo katika makutanao ya Mtaa wa Kariakoo na Jangwani,jijini Dar es Salaam.
Mzee mwenye nyumba hiyo afahamikae kwa jina la Mzee NYUMBA (kushoto) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo la tukio jioni ya leo,juu ya nia yake ya kuwatoa wapangaji wake wote waliokuwepo kwenye nyumba yake hiyo kwa madai ya kutolipia kodi ya pango kwa kipindi cha miaka mitatu.Hali hiyo imekuja kutokana na Mzee huyo kupewa kibali maalum na Mahakama baada ya kushinda kesi dhidi ya mtu aliekuwa akisema ndie mwenye nyumba na kuamua kuwaondoa wapangaji wake wote katika nyumba hiyo.Kwa Upande wa Wapangaji wa Nyumba hiyo walieleza kwamba wao hawakukaa katika nyumba hiyo bila ya kulipa kodi,kwani kuna Mtu ambaye aliwapangisha (hawakumtaja jina) kuwa ndie aliekuwa akichukua Kodi zao kwa kipindi chote hicho.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Mtaa Huo,Mzee Kasim (katikati) pamoja na majirani waliokuwepo eneo hilo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbinga Auction Mart wakiendelea na jukumu walilopewa la kutoa vyombo vya wapangaji wote waliokuwepo katika nyumba hiyo.
Vyombo vikiwa vimetolewa nje ya nyumba hiyo.
Jamaa Mbinga Auction Mart hanawa Masihara hata kidogo katika katika jukumu hili.
Vyombo vikiwa nje.
Wapangaji hao wakifanya utaratibu wa kupeleka vyombo vyao katika nyumba ya jirani ili kujistiri kwa siku ya leo.
Wakati huo huo likazuka zengwe la kupotelewa kwa simu kwa mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo na hapa ilikuwa ni kelele za kudaiana simu hiyo,maana wakati inaondoka mwenyewe alimuona huyo mwizi wake.
Mashuhuda wakiendelea kuangalia tukio hilo.
Mmoja wa Majirani wa nyumba hiyo akiwaeleza jambo Wapangaji waliotolewa katika nyumba hiyo jioni ya leo.
Mtaa mzima wa Jangwani leo ulikuwa namna hii kutokana na tukio hilo la kutolewa kwa wapangaji katika nyumba hiyo.
Picha zote kwa Hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog

No comments: