Tuesday, October 11, 2011

Nyumba na vyombo vya jambazi vyachomwa moto Iringa

Ndugu wa karibu wa mtuhumiwa wa upigaji nondo katika eneo la Kata ya Mkwawa na Mlandege katika Manispaa ya Iringa wakiwa chini ya ulizi wa polisi baada ya wananchi na polisi kufanikiwa kuvunja ngome ya ujambazi eneo la Kigamboni mjini Iringa leo (picha na Francis Godwin)

Mwananchi mwenye hasira kali mkazi wa Kigamboni kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa akivunja nyumba ya jambazi sugu Msafiri Ilomo aliyetolewa kwa msahama wa Rais na kuonyesha kuwatesa wananchi kwa kuwapiga nondo na kupora mali zao (picha na Francis Godwin)
Wananchi wa Kata ya Mwangata na kata ya Mlandege katika Manispaa ya Iringa wakitazama nyumba ya Msafiri Ilomo ikiteketezwa kwa moto baada ya wananchi kuamua kuivunja nyumba hiyo na kuichoma moto baada ya kukutwa mali mbali mbali ambazo majambazi hao walikuwa wakipora kwa wananchi baada ya kuwapiga nondo mali zenye thamani ya zaidi ya milioni 15 (picha na Francis Godwin)
Gari la polisi wilaya ya Iringa likibakia vyombo mbali mbali zinavyodaiwa kuwa ni mali za wizi ambavyo vilikutwa katika nyumba ya jambazi sugu Msafiri Ilomo mkazi wa Kigamboni mjini Iringa ,mali ambazo zinadaiwa kuporwa na kundi hilo la ujambazi baada ya kuvunja na kujeruhi wananchi mbali mbali kwa nondo (picha na Francis Godwin)

No comments: