Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini VETA, imepongezwa kwa utekelezaji kwa kasi, zile changamoto za kupanua wigo wa mafunzo inayoyatoa, na kuyaboresha kwa viwango vya kimataifa baada ya kukamilisha majengo ya kisasa ya kutolea mafunzo ya kozi mpya za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini (Tehama).
Pongezi hizo, zimetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini, Dr. Shukuru Kawambwa, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji mradi ujenzi wa vyuo vipya vine vya VETA, vya Lindi, Mayanra, Pwani na Dar es Salaam, vilivyofadhiliwa na Serikali ya Korea kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 22, sawa na Shilingi bilioni 37 za Kitanzania.
Dr. Shukuru kawambwa, amesema, ameridhishwa sana na kazi nzuri iliyofanywa na VETA, na na kukubwa zaidi ni jinsi alivyoshuhudia vifaa na mitambo ya kisasa ya kufundishia, na kueleza kuwa Tanzania kama nchi, itapiga maendeleo makubwa kwa kuwatumia wahitimu wa kozi hizi mpya. Hata hivyo, ameipa VETA, changamoto mpya ya kuongeza idadi ya wanafunzi watakaojiunga na fani hizi mpya.
Awali, akimkaribisha Waziri kwenye jengo jipya la VETA, Dar es Salaam lililopo eneo Kipawa, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Eng. Zebadiah Moshi, ameishukuru serikali ya Korea kwa kuufadhili huo mradi, na kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuiamini VETA kuutekeleza mradi huo.
Eng. Moshi amesema kuanzia sasa, VETA, itaendesha kozi 5 mpya za ICT ikiwezo, Web Design na Multi Media. Automatic Control, Electronics na Utengenezaji wa Computers. Mkurugenzi Mkuu wa Veta, pia alitoa changamoto mpya zinazoikabili VETA, ni ukosefu wa majengo ya kisasa ya kutosha kuwekewa vifaa vipya na vya kisasa vya kufundishia, walivyopokea toka nchini Korea, hivyo kuiomba serikali kugharimia ujenzi wa vyuo vingine vingi zaidi vya Veta,
Majengo hayo, yamejengwa na kampuni ya Ujenzi ya MAC na SAMMI toka nchini Korea kwa ushirikiano na kampuni ya HAINAN toka nchini ya China na Kapuni ya Ktanzania ya AQE Ltd na yamegharimu Shilingi za Kitanzania bILIONI 6.4 pamoja na vifaa vilivyomo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment