Mtuhumiwa wa ujambazi Iringa Msafiri Ilomo akiwa na mke wake ,hadi sasa mwanamke huyo yupo mikononi mwa polisi
Mtuhumiwa wa ujambazi Bw Msafiri Ilomo ambaye anasakwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na mali za wizi jana eneo la Kigamboni Iringa
Mmoja kati ya majeruhi waliokatwa mkono na kikundi hicho cha majambazi Bw Michael Chengula akiuguza jeraha
Diwani wa kata ya Mwangata Galus Lugenge akionyesha eneo ambalo Marehemu Damas Kisinga aliuwawa kwa kupigwa nondo na majambazi hao na kupokonywa simu yake iliyokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi Msafiri Ilomo
Hapa ndipo alipouwawa Damasi Kisinga na watua hao ni eneo la Chuo cha Donbosco mjini Iringa
Cheti cha ndoa cha Maneno Ezekiyeri na Bahati Mohamed wa Ilala ni miongoni mwa vitu vilivyokutwa eneo la tukio
Nguo wa waumini wa kiislam ambazo zimeshindwa kutambuliwa
Nguo za ndani za wanawake zikizagaa wakati wa utambuzi wa mali za wizi zilizokutwa katika nyumba ya jambazi eneo la Kigamboni mjini Iringa
Bendera hii ya CCM pia iliibwa ,inaonekana majambazi hao walikuwa hawaachi kitu ,japo kwa bendera ni vigumu kutambua mmiliki halisi
Mali zote hizi ni za wizi
Wananchi wakitambua nguo zao kituo cha polisi
Wananchi wa Manispaa ya Iringa mchana huu wanaendelea kutambua mali zao mbali mbali ambazo zikikutwa jana eneo la Kigamboni katika nyumba ya Msafiri Ilomo ambaye anadaiwa kumiliki mtandao wa ujambazi .
Wananchi wengi wameonyesha kukata tamaa kuendelea na kutambua mali zao baada ya kukosa ushahidi wa uhalali wa mali hizo baada ya wengi kufika kituo cha polisi bila ya risti za mali zao ,huku baadhi yao wakidai kukosa mali zao ambazo ziliibwa na wezi hao .
Baadhi ya vituko ambavyo vimejitokeza ni pamoja na kuwepo kwa nguo za ndani nyingi ambazo zinasadikika kuwa wezi hao walikuwa wakianua katika nyumba za wananchi ,pia bendera na skafu wa CCM pamoja na vitu vingine ambavyo ni mali ya makanisa na misikiti vimekutwa wakati wa utambuzi wa mali mbali mbali.
Wakati huo huo mmoja kati ya wanawake waliofika kutambua mali zilizoibwa ameueleza mtandao huu kuwa amepata kutambua nguo zake za ndani ambazo zilichukuliwa nawezi hao bafuni ,pamoja na nguo nyingine zilizokuwa zimeanikwa nje .
Habari na Picha na mwandishi wetu Francis Godwin
No comments:
Post a Comment