Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete amewataka watendaji wa Serikali yake kufanya uamuzi wa haraka kukabiliana na tatizo la umeme nchini akisema haoni kama kuna kasi ya uhakika katika kukabiliana na suala hilo.
Akizungumza katika kikao na watendaji hao alichokiitisha Ikulu, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete aliwataka watendaji hao kufanya uamuzi bila ya kuwa na kigugumizi kwa manufaa ya wananchi wakitambua kuwa nchi iko katika hali ya dharura kubwa ya upatikanaji wa nishati hiyo.
“Tuko katika hali ya dharura. Sioni hisia za haraka za kuchukua uamuzi na hatua nyingine muhimu za kukabiliana na dharura ya upatikanaji wa umeme. Hatuwezi kuendeleza kuwa na kigugumizi katika kuchukua uamuzi wa kuitoa nchi katika changamoto kubwa hizi za upatikanaji wa nishati,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Ubwana mkubwa wa kila mmoja wetu utatambuliwa kutokana na mafanikio ambayo kila mmoja wetu ataonyesha katika kukabiliana na hali hii ya upatikanaji wa nishati.”
Rais Kikwete pia amewataka watendaji hao kuelekeza nguvu zao kwa kufanya kazi kwa karibu zaidi na wawekezaji ambao wamethibitisha umakini wao katika uzalishaji umeme. Soma zaidi kwanzajamii.com
No comments:
Post a Comment