Mimi ni mteja wa Tigo na nimekuwa na namba ya TIGO kwa muda mrefu sasa na mara nyingi nimekuwa sifurahii huduma wanazotupa sisi wateja wao maana inaonekena kwao “mteja si mfalme” kwao “mteja ni fala”
Alhamis tarehe 13/10/2011 majira ya saa 3 usiku nilitumia huduma yao ya TIGO PESA kununua umeme wa luku wa TZS.11,000.00 lakini cha kushangaza sikupata umeme nilionunua Kilichonikera zaidi ni kuwa baada ya kukosa huo umeme nilipiga namba ya Customer service (071
3800 800) bila mafanikio mpaka nilipokwenda kulala saa 5 hivi usiku Siku ya pili 14/10/2011 niliendelea kutafuta namba ya customer service mpaka ilipofika saa 7 mchana ndipo ilipopatikana na kuambiwa nipige namba 150 ambayo baada ya takriban saa nzima ilipokelewa na kijana aliyeipokea hatujitaja jina kama inavyotakiwa na akaniambia nimpigie baada ya
masaa 2 tatizo langu litakuwa limeshughulikiwa na kwamba wameshachukua namba yangu Baada ya masaa 2 nilipiga tena na kama ilivyo kawaida yao ilichukua zaidi ya saa nzima kupokea na ilipopokelewa niliambiwa kuwa ujumbe wa namba zangu za luku nitatumiwa lakini cha kusikitisha ni kwamba mpaka leo tarehe 17/10/2011 sijapata pesa yangu wala huo umeme niliahidiwa Kitu kimenipelekea kuandika hivi ni kutokana na ukweli kwamba hii nimara ya pili kwa kisa kama hiki kunitokea mara ya kwanza pesa haikuwa nyingi lakini hii ya sasa inauma na kama kuna mtu anataka kulithibitisha hili nipo tayari kumpatia namba yangu ahakikishe wizi huu uliokithiri
WANAJAMII WENZANGU HUU SI “WIZI WA MCHANA UNAOFANYA NA HAWA TIGO?” NAOMBA
MNISHAURI NIFANYEJE ILI NIRUDISHIWE PESA YANGU
Monday, October 17, 2011
YALE YALE “TIGO NA UBABAISHAJI / WIZI WAO”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment