Tuesday, November 1, 2011

Dr Shein azindua tawi la benki ya wananchi wa zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Chake chake Pemba wakati wa uzinduzi wa tawi la benki ya wananchi wa Zanzibar PBZ, Pemba,ambapo huduma ya ATM pia itapatikana kwa saa 24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Kaimu Waziri wa Fedha Dk Mwinyihaji Makame,akitoa nasaha kwa wananchi na kuwataka kuweka fedha zao katika benki ya watu wa Zanzibar tawi la Chake chake leo,wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akitoa pesa kwa kutumia huduma ya ATM mara baada ya kulizindua Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akionesha pesa alizotoa kupitia matandao wa ATM kwa benki ya watu wa Zanzibar PBZ,baada ya kuzindua rasmi tawi jipya la chake chake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akijaza fomu ya kujiunga na benki hiyo mara baada ya kulizindua Tawi jipya la PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akitia saini fomu za kuweza kupatiwa ATM card ya kutolea pesa katika Benki ya watu wa Zanzibar katika sehemu lilipo tawi la Benki hiyo,wakati wa uzinduzi wa tawila PBZ Chake chake Pemba jana,(kushoto) Mkurugenzi mtendaji Juma Amour.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Amour,wakati wa sherehe za uzindu wa Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar PBZ,wilaya ya Chake chake Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wasoma utenzi wakati wa uzinduzi rasmi w2a tawi la PBZ leo huko Chake chake Pemba.Picha na Ramadhan Othman Pemba.

No comments: