Musa Juma,
Arusha MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemuomba Mkuu wa Gereza kuu la Arusha, kumruhusu kuwalipia faini wafungwa 22 wanaotumikia vifungo vya makosa mbalimbali katika gereza hilo kutokana na kushindwa kulipa faini zao. Katika barua yake jana yenye orodha ya wafungwa hao kwa mkuu huyo wa gereza, Lema alieleza kuwa ofisi yake ya jimbo inataka kuwalipia faini wafungwa hao ambao wengi wamefungwa kwa makosa madogo na kushindwa kulipa faini. "Wafungwa hawa licha ya kusababisha msongamano, vifungo vyao vinatokana na ukweli kuwa Watanzania hao walishindwa kulipa faini na sio kwa ridhaa yao bali kutokana na hali duni ya maisha yao," ilisomeka sehemu ya barua hiyo. Lema ambaye bado yupo rumande katika gereza hilo, baada ya kugoma kuwekewa dhamana katika kesi ya kufanya maandamano na mkusanyiko bila kibali, alisema ofisi yake, inaomba kupatiwa majina yote ya wafungwa waliokosa faini walizotakiwa kulipa ili afanye utaratibu wa kuwatoa kwa kuwalipia faini hizo katika chombo husika.
"Nitafurahi utekelezaji huu kufanyika haraka ili kupunguza msongamano katika gereza hili na wafungwa hao kujumuika na wananchi wengine katika shughuli mbalimbali za maendeleo," alisema Mbunge Lema katika barua hiyo. Hadi jana tayari majina ya wafungwa 22 ambao wanatumikia kifungo baada ya kushindwa kulipa faini kati ya Sh 10Milioni na Sh200,000 yalikuwa yamepatikana. Wafungwa hao ni Rasul Hemed mwenye namba 262/2011,Hamis Jafari455/2011, Gabriel Martin105/2011, Simon Peter503/2011 na Emanuel Ndelekwa namba 400/2011. Wengine namba zao kwenye mabano ni Juma Seleman (60/2011)Bakari Ramadhani (354/2011) Ally Ramadhani (300/2011), Sakidi Athuman 305/2011) na Charles Mkama (555/2010). Wafungwa wengine ni Emanuel Bundala (457/2011) Mdoo Saruni (337.2011), Rajab Ally(450/2011), Lameck Abdiel (362/2011) Abdul Ismail (439/2011), Anold Philipo mwenye namba315/2011. Wengine ni Julius Ngadayo (377/2011),Ombeni Stephano (475/2011), Ney Sabas(111/2011), Bura Thomas(59/2011) na Emanuel Samweli (714/2007). Mwenyekiti wa mfuko wa Maendeleo wa Jimbo la Arusha (ARDF), Elifuraha Mtowe, alisema jana kuwa baadhi ya wananchi wameanza kutoa michango ili kufanikisha mpango wa kutoa gerezani wafungwa hao. Mgomo wa mabasi wasitishwa Hatimaye mgomo wa mabasi yanayotoa huduma ya usafiri jijini Arusha, maarufu kama ‘vifodi’, ulisitishwa jana na kuanza kutoa huduma kama kawaida. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia jana katika kituo cha mabasi na vituo vidogo magari hayo yakiwa yanaendelea na kazi ya kubeba abiria. Baadhi ya madereva waliozungumza na Mwananchi walieleza kuwa, licha ya baadhi yao kumuunga mkono Lema kutokana na kupinga vitendo vya polisi na viongozi wengine wa usalama kutisha raia na kuwafungulia kesi kwa malengo ya kisiasa, wengine walisitisha huduma kwa kuogopa magari yao kuvunjwa vioo. "Isingewezekana jana kutoa huduma magari yalikuwa yakitishiwa kuvunjwa vioo na vijana wanaodaiwa kuwa wa Chadema, sasa tuliona badala ya kupata hasara ya vioo bora tusitishe huduma," alisema Bakari Msangi. Waliohamasisha mgomo kusakwa. Jeshi la Polisi mkoani hapa, linaendelea kuwasaka vijana wanaotuhumiwa kuchochea mgomo wa mabasi uliotokea juzi na kusababisha adha kubwa kwa abiria wakiwemo wanafunzi. Hadi juzi jioni zaidi ya vijana 30 walikamatwa kuhusiana na vurugu hizo.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Akili Mpwapwa, alisema jeshi hilo haliwezi kuachia watu wakiendelea kuchochea vurugu jijini Arusha. "Tunaendelea na uchunguzi na kuwasaka wote waliochochea mgomo na kufanya vurugu. Ingawa tayari tumewakamata baadhi yao, uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani," alisema Mpwapwa. Mbunge Lema alipelekwa mahabusu mapema wiki hii baada ya kukataa kuwekewa dhamana katika kesi inayomkabili ya kuandamana bila kibali na kuwafanya wafuasi wake wakiwemo madereva wa vifodi kusitisha shughuli zao juzi na kwenda kumtembelea gerezani.

No comments:
Post a Comment