Monday, December 26, 2011

JESHI LA POLISI IRINGA KUMLIPA KAMERA MWANDISHI WA ITV IRINGA

Bw.Laurian Mkutamba
Na Francis GGodwin- Iringa

Jeshi la polisi mkoani Iringa limetoa siku mbili kuanzia leo, kulipa kamera ya mwandishi wa habari wa habari wa ITV.

Mwandishi huyo Laurent Mkumbata alivunjiwa kamera yake na OCD wa wilaya ya Iringa, wakati wa vuguvugu la misukule lililovuma hivi karibuni kwa kwa Mbilinyi maeneo ya Ferelimo manispaa ya Iringa.

Mwandishi wa mtandao huu Shabany Lupimo kutoka Iringa anaripoti kuwa ,kamanda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo, Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Iringa, Evarist Mangalla, amewahakikishia waandishi hao kuwa ndani ya siku hizo OCD huyo atamlipa kamera yake mwanahabari huyo, ambayo itakuwa na ubora na uwezo sawa na ile aliyokuwa anafanyia kazi hapo awali.

Katika vuguvugu hilo la misukule watu kadhaa wakiwemo wa waandishi wa habari na askari wa jeshi la polisi walijeruhiwa kwa mawe na wananchi, na polisi kulazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatuliza.

Vuguvugu hilo lilitokea baada ya polisi na waandishi wa habari kuingia ndani ya nyumba ya mama huyo ili kuona kama kweli kuna misukule na kuikosa, ambapo wananchi walianza kuwarushia mawe kwa madai kwamba walipokea rushwa.

Pamoja na hayo pia ametumia mwanya huo, kuwahakikishia amani na usalama wa maisha na mali zao wakazi wa Iringa, wakati wa kusherekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya, kwa kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kukabiliana na watu watakaosherekea sikukuu hizo kwa kuvunja sheria za nchi.

Hata hivyo amewataka kuchukua tahadhari ya ulinzi kwenye nyumba zao ili kutowapa fursa wezi, na pia kushirikiana na jeshi hilo ili kuwabaini waharifu.

Aidha amewataka madereva kutoendesha gari wakiwa wamelewa au kuwapa watu wasio na sifa za kuendesha vyombo vya moto kuendesha magari, ili kuepuka ajali zisizo za lazima, na kwamba atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatu za kisheria.

Katika hatua nyingine amewatahadharisha wazazi kutowaruhusu watoto wao kushiriki disco toto, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea, kama ilivyowahi kutokea mkoani Tabora, ambako watoto zaidi ya 16 walipoteza maisha kwenye ukumbi wa disco kutokana na kukosa hewa.

No comments: