Tuesday, December 20, 2011

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI ARUSHA YAAHIRISHA KESI YA CHADEMA

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imeahirisha kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dkt.Wilbroad Slaa na wafuasi wa chama hicho hadi January 17 mwakani kwa madai kuwa shtaka la 1,4,7 lina kasoro
Akiahirisha kesi hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Magesa Charles amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria za mwenendo wa kesi za jinai namba 234 mahakama hiyo inaamuru kuwa hati ya mashtaka ifanyiwe marekebisho kabla ya hukumu.
Magesa alisema kuwa ombi lililotolewa na wakili wa upande wa mashtaka Issa Rajabu kuomba tafsiri ya makosa kuwa washtakiwa wamekuwa wakifunguliwa kesi mahakamani zinazofanana hivyo alinukuu kutoka kifungu 234 kuwa si sahihi mahakama kutoa tafsiri kisheria kwa kuwa mahakama hiyo ni ya hakimu mkazi na sio mahakama kuu na makosa yanayowakabili washtakiwa yatatolewa tafsiri pindi ushahidi utakapokamilika kwa kutumia kifungu na kosa .
Aidha Magesa alisema kuwa hati ya mashtaka ina upungufu wa kwa kuwa haiainishi makosa yaliyotendwa na washtakiwa,pamoja na kuna makosa madogo madogo ya kimaandishi juu ya sehemu tukio lilipotokea na kutotajwa jina afisa aliyeaamuru wananchi kutawanyika katika viwanja vya NMC
Kesi hiyo ni ya maandano yaliyopelekea vifo vya watu 5 yaliyofanyika tar.5 january 2010 ambapo imeahirishwa kwa ajili ya marekebisho ya hati ya mashtaka.
Wakati huohuo mahakama ya hakimu mkazi Arusha imetaja kesi ya Mkesha wa Ukombozi iliyokuwa inawakabili wafuasi 26 wa CHADEMA na viongozi wa chama hicho Freeman Mbowe,Tundu Lisu ,Wilbroad Slaa mpaka hapo January 27 kwa kuwa upelelzi umeshakamilika.
Akitaja kesi hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Devotha Kamuzora alisema kuwa kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe iliyopendekezwa ambapo alimtaka mdhamini wa mshtakiwa Tindu Lisu kutoa maelezo ya sababu iliyosanbabisha mshtakiwa huyo kutofika mahakamani hapo.
Mdhamini wa Tindu Lisu anayefahamika kwa jina la Kalist Lazaro aliiomba mahakama ipokee udhuru wa mshtakiwa kwa kuwa alimpigia simu na kumuagiza kufika mahakamani kwa kuwa alikuwa anaumwa.
Hakimu Devotha aliimtaka mshtakiwa pindi atakapofika mahakamani hapo kwenda na vithibitisho kutoka kwa daktari kuwa alikuwa anaumwa ambapo aliiahirisha kesi mpaka January 23 mwaka 2012.

No comments: