Friday, December 23, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATEMBELEA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hadi sasa tayari jumla ya Maiti 38 zimekwisha opolewa majini na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na 19, kati yake mpaka sasa bado haziweza kutambuliwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo.
Baadhi ya wananchi walio katika Kambi hiyo, wakifua nguo zao kambini hapo.
Mmoja kati ya watoto waishio katika Kambi hiyo ya Klabu ya Yanga, akiwa ameuchapa usingizi katika eneo ambalo linatumika kufulia nguo, wakati mama yake akifua nguo zake mahala hapo.
Picha ya juu inaoonyesha sehemu iliyoathirika na mafuriko hayo.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akitelemka katika Helkopta, baada ya kuzunguka hewani na kujionea athari zilizotokea katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo.
Picha na Sufian Muhidin

No comments: