Wednesday, December 28, 2011

Mbunge Wa Wawi(CUF)Hamad Rashid Aigomea Kamati ya Nidhamu na Maadili ya CUF

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF)akiongea na Waandishi wa Habari Jana
--



MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) ameigomea Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kumhoji na kumjadili kuhusu tuhuma zinazomkabili za kukiuka Katiba, akidai hana imani na wajumbe wake. Pia ameigomea kwa kudai kuwa tayari alishafahamu kwamba Kamati hiyo ilikuwa na maamuzi ya kumfukuza uanachama, kupitia barua pepe aliyoinasa ikitoka kwa Katibu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwenda kwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba.



Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mh Hamad ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF alisema alipokea barua ya kuitwa kuhojiwa kwa tuhuma za kwenda kinyume cha Katiba ya CUF, Desemba 23, mwaka huu na kikao hicho kilifanyika rasmi jana.



Alisema baada ya kuhudhuria kikao hicho, alilazimika kukigomea kuendelea kumjadili kutokana na kutokuwakubali wajumbe watano kati ya wanane akiwemo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali na Katibu wake Hamis Hassan.



Alisema viongozi hao wawili amewakataa kutokana na ushiriki wao katika kumtuhumu. Alisema hana imani na Machano baada ya kiongozi huyo kuahidi kumshughulikia katika kikao kilichofanyika hivi karibuni bila ya kumpa nafasi ya kusikiliza upande wake.



No comments: