Sunday, December 4, 2011

Mwanahabari wa siku Nyingi,Alfred Ngotezi afariki Dunia

Hayati Alfred Ngotezi
Habari iliyotufikia hivi punde na yakuaminika kabisa,inaeleza kuwa Afisa Uhusiano Mwanzamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na aliekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Serikali la Kila siku (Daily News),Alfred Ngotezi amefariki Dunia ghafla asubuhi hii Jijini Arusha ambako alikuwepo kwa maandalizi ya Mkutano wa Mashirika ya Afrika ya Hifadhi za Jamii unayotaraji kuanza rasmi kesho kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha.

Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa hii,anaeleza kwamba Hayati Ngotezi kabla ya kuaga Dunia alikuwa katika meza ya chakula na baada ya muda kidogo akanyanyuka kwa nia ya kwenda kujisaidia na hapo ndipo alipoanguka ghafla na kupoteza maisha.

Globu ya Jamii inaungana na wadau woote walioguswa na msiba huu mzito wakiwemo Ndugu,Jamaa na Marafiki katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Alfred Ngotezi mahala pema peponi

-Amin.

No comments: