Friday, December 23, 2011

Rais Kikwete awakumbuka watoto wanaoishi mazingira hatarishi, Singida

Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Parseko Kone, kwa niaba ya Rais Dk.Jakaya Kikwete, akikabidhi zawadi ikiwemo mchele na mbuzi wawili kwa ajili ya kituo cha Malezi Kititimo kilichopo mjini Singida, kwa ajili ya watoto hao kusherehekea vizuri sikukuu ya Krismasi,Watoto hao wanaishi mazingira hatarishi, wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya Singida Paschal Mabiti na kulia kabisa ni kaimu mkurugenzi manispaa Singida, Simon Hoja.

Singida,Desemba 23,2011.
RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya sikukuu ya Krismasi, kwa ajili ya watoto wanaolelewa na kituo cha Malezi Kititimo, kilichopo Mjini Singida.

Zawadi hiyo ya Krismasi kwa kituo hicho, imetolewa jana ijumaa, na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone, kwa niaba ya Rais Dk.Jakaya Kikwete.

Akikabidhi zawadi hizo, Rais Dk.Kikwete amewatakia kila la heri watoto hao, katika kusherehekea sikukuu hiyo, na anawaomba wajione sawa na watoto wengine duniani katika Krismasi hiyo.

Msaada huo wa chakula uliotolewa ni mchele kilo 60, mafuta ya kupikia dumu moja kubwa, mbuzi wawili na viungo mbalimbali kwa ajili ya mapishi,vyote vikiwa na thamani ya Sh.550,000.

Mkuu wa mkoa Singida, Dk.Kone, naye aliunga mkono msaada huo kwa kutoa katoni moja ya juisi, boksi moja la biskuti na mifuko ya pipi.

Wakitoa shukrani hiyo, watoto hao walimshukuru Rais Kikwete kwa kuwakumbuka kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

No comments: