Wednesday, December 7, 2011

RAIS WA ZANZIBAR AKITEMBELEA JUMBA LA ZAMANI.

Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akiangalia na kupata maelezo ya namana ya kutengeneza gazeti katika chumba cha habari cha gaazeti la Zanziba Leo wakati alipotembelea jengo hilo.J


PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohd Shein akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo zanzibar Yussuf Omar Chunda wakati alipolitembelea jumba la zamani la kurushia matangazo ya redio hapo rahaleo mjini zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo zanzibar Yussuf Omar Chunda kulia ambae akitoa maelezo ya jumba la zamani la kurushia matangazo ya redio hapo rahaleo wakati Rais alipolitembelea jengo hilo.
Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amesema kuwa Jengo la Zamani la iliyokuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar lazima lirejeshwe katika hadhi yake ya zamani ili liweze kutumika katika maswala mbalimbali ya Sanaa.
Amesema kuwa Jengo hilo lina historia kubwa sana kwa upande wa Zanzibar na Jengo ambalo ni madhubuti na lipo katika sehemu nzuri hivyo kurejeshwa kufanya kazi kama zamani ya kuonesha michezo ya kuigiza na kutumika kwa maonesho ya Vikundi vya Taarabu litarejesha hadhi na haiba katika Zanzibar.
Dk. Shein ameyasema hayo hivi leo wakati alipolitembelea Jengo hilo ili kuona juu ya matumizi yake ya hivi sasa na hali lilivyo kutokana na historia kubwa ya Jengo hilo kwa Zanzibar.
Amesema kuwa Shirika la Gazeti la Serikali Zanzibar linalochapisha Gazeti la Zanzibar Leo katika Jengo hilo litatafutiwa sehemu nyingine nzuri na kubwa ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi na Jengo hilo kuacha kutumika kwa ajili ya sanaa.
Akizungumzia juu ya suala la iliyokuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar amesema kuwa imefika wakati kwa uongozi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kuandika historia ya kuanzishwa Redio hiyo ambayo ni ya mwanzo katika Afrika Mashariki.
Dk. Shein amesema kuwa si vizuri kwa Redio hiyo kuwa ya mwanzo kuanzishwa wakati historia yake haionekani wala haipo hivyo ni wajibu viongozi wa Shirika hilo kuchukua kila juhudi kuona kuwa wanaindaika historia ya kuanzishwa kwa Redio hiyo pamoja na viongozi wake kuwekewa kumbukumbu za picha wakiwemo watangazaji wake.
Aidha Dk.shein ameutaka uongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo kulienzi na kulidumisha Jengo hilo kwa kulifanyia matengenezo kwani amesema kuwa hivi sasa huwezi kupata jengo madhubuti na lenye haiba yake hilo.
Akizungumzia juu ya Habari Maelezo Zanzibar amesema kuwa hatua iliyochukuliwa ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Maktaba itasaidia sana katika uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu za matukio mbalimbali za Picha,Magazeti na Majarida.
Mapema Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda alimuelezea Rais Shein historia ya Jengo hilo na matumizi yake ya hivi sasa.

No comments: