Afisa Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCAT) Joseph Kanyunyu akitoa ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana jijini Dar es salaam juu ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mfuko huo wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
-Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Sera Wizara ya Fedha Joseph Kiraiya akitoa ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana jijini Dar es salaam juu ya mafanikio mbalimbali ambayo Wizara hiyo imeyapata katika kuwaletea maendeleo wananchi wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) Mordgard Lumbanga akitoa ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana jijini Dar es salaam juu ya mafao mbalimbali yatolewayo na mfuko huo wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Afisa Mauzo wa Benki ya Posta David Philipo akitoa ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana jijini Dar es salaam juu ya huduma ya Benki Popote inayotolewa na Benki hiyo wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana mawazo jana jijini Dar es salaam na Katibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi akiangalia kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika kikiwaburudisha wananchi jana jijini Dar es salaam waliotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
No comments:
Post a Comment