Thursday, December 22, 2011

Taswira Za Ziara Ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein,akizugumza wafayakazi wa ujenzi wa barabara ya Chanjamjawiri –Tundauwa jana,inayojengwa na Idara ya ujenzi ya Wizara ya Miundombinu kwa mashirikiano na ufadhili wa Norway.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein,akiuliza suala kwa Msaidizi Meneja wa ZSTC Pemba Hamad Khamis Hamad,alipotembelea maghala ya karafuu MKoa wa Kusini Pemba huko Bandarini ya Mkoani jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein,akizungmza na Msaidizi Meneja ZSTC Pemba Hamad Khamis Hamad, alipofanya ziara ya kutembelea maghala ya karafuu Mkoani Pemba jana,pia kujua matatizo katika utekezaji wa zao hilo la Uchumi wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein,akitoa ushauri kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Chanjamjawiri –Tundauwa Faki Juma Khamis,(wa nne kulia)alipofanya ziara ya kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, inayojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Norway jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mahamed Shein,akimpa maelekezo Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe Masoud Hamad Masoud,alipotembelea Barabara ya Mizingani-Wambaa Mkoa wa Kusini Pemba,alpokuwa katika zia ziara maalum kisiwani humo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-ZanzibarNo comments: