Friday, January 20, 2012

CCBRT YAHITIMISHA MPANGO WA WAELIMISHAJI RIKA WENYE ULEMAVU

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans, akifafanua jambo katika mkutano wa kuhitimisha mradi wa kuwawezesha Waelimishaji Rika wenye Ulemavu kuwa waelimishaji kwa walemavu wenzao juu ya vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi, jiji Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi akizungumza katika mkutano huo.
Mwelimishaji Rika, Neema Abas kutoka Ngamiani Tanga,mwenye ulemavu wa kutosikia, akichangia hoja katika mkutano huo.
Mwelimishaji Rika Farida Chamwana kutoka Kilosa Morogoro, akitumia lugha ya alama kuchangia hoja wakati wa mkutano huo.
Meneja Mradi wa CCBRT, Clement Ndahani, akijibu maswali mbalimbali yaliyoelekezwa upanda wao na watu wenye ulemavu waelimishaji rika leo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Vitalis Makayuga akichangia hoja na kuomba CCBRT isisitishe mpango huo ili walemavu waendelee kuelimika juu magonjwa hayo.
Hamis Mchuro ambaye ni Muelimishaji Rika kutoka Kijitonyama, akiipongeza CCBRT kwa kuwezesha waelimishaji rika walemavu nchini
Baadhi ya Watu wenye Ulemavu wakiwa katika mkutano wa kuhitimisha mradi wa kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kuwa waelimishaji kwa walemavu wenzao juu ya vita dhidi ya maambukiz.
Picha na Richard Mwaikenda

No comments: