Sunday, January 15, 2012

Kamati Ya Kombe La Mapinduzi Zanzibar Yakutana na Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipokea ripoti ya kamati ya mapinduzi Cup 2012 na Katibu wa Kamati hiyo Khamis Abdulla Said,wakati wa wajumbe wa kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia) akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Kampuni ya Zanzibar Ocean View Hotel,Hania Makungu,kwa uchangiaji wa Hateli hiyo katika mashindano ya mchezo mpira wa Miguu Mapinduzi Cup, yaliyomalizika hivi karibuni wakati wa Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,katika hafla hiyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,(katikati) Mohamed Raza Mwenyekiti wa kamati ya Mapinduzi Cup 2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia) akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Kampuni ya Multi-Color Printertersm Rahim Bhaaloo, cha uchangiaji katika mashindano ya mchezo mpira, Mapinduzi Cup 2012 yaliyomalizika hivi karibuni wakati wa Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,(katikati) Mohamed Raza Mwenyekiti wa kamati ya Mapinduzi Cup 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya wajumbe wa Mapinduzi Cup 2012 Mohamed Raza,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia) wakati kamati hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar Kuonana na Rais .
Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,Abdilah Jihadi Hassan,akiwatambulisha wajumbe wa kamati ya Mapinduzi Cup 2012 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na kamati hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Mapinduzi Cup 2012 chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Raza (watatu kushoto) baada ya hafla ya kuwazawadia vyeti wafadhili wa mashindano ya mchezo huo, yaliyomalizika hivi karibuni wakati wa Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,wakati wa hafla hiyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Picha na Ramadhan Othman,IKULI-ZanZibarNo comments: