Tuesday, January 10, 2012

Tendwa asema CUF ifutwe

AITAKA IREJEE AMRI YA MAHAKAMA, ASEMA ADHABU YA KUIDHARAU NI KUFUTWA
Waandishi wetu MSAJILI wa Vyama vya siasa nchini, John Tendwa amekionya Chama cha Wananchi (CUF), kwa kuendesha kikao kilichowajadili na kuwafukuza Hamad Rashid Mohamed na wenzake wakati kimepewa amri na Mahakama Kuu ya kutofanya hivyo huku akikitaka kirejee na kutii amri hiyo.Kauli ya Tendwa imekuja siku moja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema kusema kitendo hicho cha CUF kuendesha kikao hicho ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi.
“Sijaiona amri ya mahakama (court order) inayowazuia CUF kuendelea na mkutano wao, lakini ninasema kuwa kuna uhalali wa kuwapo kwa tukio hilo? Ushauri wangu ni kwamba CUF warudi kutekeleza amri ya mahakama,” alisema Dar es Salaam jana na kuongeza:
“Mahakama ni mhimili wa Serikali wenye mamlaka kamili ya Katiba ya nchi. Mahakama imefanya uamuzi unaopaswa kuheshimiwa.” Alitaja baadhi ya makosa ambayo chama kinaweza kupoteza sifa ya kuwa chama cha siasa kuwa ni pamoja na kukiuka Katiba ya nchi, kuwa na siasa za upande mmoja na kufanya siasa zinazochochea vurugu. Barua kutoka CUF Kuhusu barua kutoka CUF, Tendwa alisema ofisi yake haijapata barua yoyote ya chama hicho inayoeleza kuhusu uamuzi wa kumfukuza uanachama Hamad Rashid na wenzake. “Mimi sijaona barua kutoka CUF inayohusu kufukuzwa uanachama kwa Hamad na hata ingekuwa imepelekwa Ofisi za Bunge ningefahamishwa,” alisema Tendwa. Tendwa alisema sababu zinazotolewa na CUF kuwa Hamad Rashid alikuwa akifanya mikutano kinyume na taratibu za chama, hazina mashiko kwa kuwa hakuna kosa kwa mbunge kufanya mkutano wa hadhara na wananchi. “Hakuna kosa kwa mbunge aliyechaguliwa na wananchi kufanya mkutano mahali popote katika nchi na kutoa msaada, si lazima kuomba ruhusa kwa yeyote wakati akitekeleza jukumu hilo,” alisema Tendwa. Aonya vyama Tendwa alivionya vyama vya siasa kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo badala ya kufukuzana uanachama akisema mfumo huo ndiyo unaoweza kujenga vyama hivyo na kuvipatia uwezo wa kukubaliwa na wananchi na kupewa dhamana ya kuongoza nchi. “Mfano, leo hii CUF wanachama wake wanarudisha kadi kwa tukio la Hamad… huku ni kukidhoofisha chama,” alisema Tendwa. Hamad: Sijapewa barua Kwa upande wake, Hamad Rashid alisema bado hajapewa barua ya kufukuzwa uanachama lakini akasema kwamba viongozi wa CUF wamepeleka barua ya kutomtambua katika Ofisi ya Bunge. Alisema hadi jana alikuwa hajapokea barua yoyote inayoonyesha kufukuzwa uanachama, jambo alilodai ni kinyume cha kanuni na taratibu za kumvua mtu uanachama. “Mpaka sasa sijapokea barua ya kunivua uanachama lakini, nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa viongozi wa CUF wamepeleka barua ya kutonitambua kwa Spika wa Bunge,” alisema Hamad....www.mwananchi.co.tz

No comments: