Wednesday, January 4, 2012

WAZIRI MAGUFULI ATOA TAARIFA KUHUSU MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA KILWA – AWAMU YA PILI .


Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli (MB) leo ametoa taarifa ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mh. Masaki Okada iliyohusu Mradi wa Upanuzi wa barabara ya Kilwa kwa Awamu ya pili.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mh. Magufuli ameelezea hatua iliyochukuliwa na Wizara yakekwa Pamoja Balozi wa japan ya kuunda Kikosi Kazi cha Pamoja kilichochunguza kuharibika mapema kwa barabara ya Kilwa hasa katika sehemu iliyojengwa katika Awamu ya Pili ya Mradi huo.

Aidha amefafanua kuwa mpango wa Mkandarasi wa kuanza matengenezo ya barabara hiyo ni mwezi Mei 2012 baada ya kipindi cha mvua.

No comments: