Sunday, February 19, 2012

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI YA CPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe.Request Muntanga (katikati) akiendesha kikao cha kamati ya Bajeti ya CPA Kanda ya Afrika kilichofanyika katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika ambae pia ni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah na wa kwanza kushoto ni Mhasibu wa CPA Kanda ya Afrika ambae pia ni Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge Tanzania, Nd. George Seni.
Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika Dar es salaam kwa lengo la kujadili hali ya kifedha ya Chama hicho hususan mapitio ya bajeti (re-allocation) yanayohitajika ili kukidhi mahitaji ya kifedha katika robo mwaka inayokuja. Bunge la Tanzania ndio makao makuu ya Sekretarieti ya Chama hicho barani Afrika ambapo jumla ya mabunge 19 ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ni wanachama na pia kuna mabaraza ya kutunga sheria 45 katika Kanda ya Afrika ikiwemo Baraza la Wawakilishi Zanzibar yanayohudumiwa na Sekretarieti hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya CPA Kanda ya Afrika wakifuatilia mjadala katika kikao chao kilochomalizika Jumapili katika hoteli ya Whitesands, kutoka kushoto ni Mjumbe kutoka Uganda, Mhe. Elijah Okupa, na mjumbe kutoka Swaziland Mhe. Seneta Winnie Magagula na Mjumbe kutoka Tanzania Mhe. Zitto Kabwe, wa kwanza kulia ni Mhasibu wa CPA Kanda ya Afrika ambae pia ni Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge Tanzania, Nd. George Seni.
Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

No comments: