Monday, February 27, 2012

WAZIRI MAGUFULI:TANZANIA BADO INAKABILIWA NA TATIZO LA MAKAZIWaziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya tatizo la Makazi ya Wananchi wake pamoja na watumishi wa umma
Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo mjini Arusha jana wakati wa kuweka Jiwe la Msingi laMsingi wa Majengo Mawili ya ghorofa 10 yanayojengwa na Serikali kupitia wakala wa Majengo(TBA) Mkoa wa Arusha
Majengo hayo yanatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 10.2 yakikamilika ambapo hadi sasa ujenzi wa Majengo hayo umegharimu shiliningi bilioni 5.2
Waziri Magufuli amewambia wananchi walioshuhudia uwekeji huo wa jiwe la Msingi kwamba asilimia kati ya 70 na 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi katikamakazi holela
Dkt Magufuli amefafanua kuwa hadi sasa Tanzania inamahitaji ya zaidiya nyumba Milioni tatu kwa ajiliya makazi ya watu katika maeneo mbalimbali ya nchi
Waziri huyo wa Ujenzi Dkt Magufuli amesema tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 Serikali ilikuw ainatoa hudumaya makazi kwa watumishi wake kwa asilimia tatu tu (asilimia 3 tu) hatua ambayo imeababishakuwepo na mahitaji makubwaya nyumba za makazi kwa watumishi wake
Waziri Magufuli pia amesema Serikali kupitia wakala wa Majengo hapa nchini inatarajia kujenga nyumba zaidi ya 10,000 kwa ajili ya makazi ya watu wakiwemo watumishi wa umma mwaka huu wa feha 2011 / 2012
Ameahidi Wizara yake kutoa kiasi cha shilingi bilioni tano ili wakala wa majengo Mkoani Arusha Taasisi hiyo imeweze kukamilisha
majengo hayo haraka
Amesema maslahi ya watumishi hayo ni lazima yafanane na kazi nzuri inayofanywa na wakala wamajengo likiwemo suala la kuwapandisha vyeo watumi wote wa wakala wa majengo hapa nchini na marupurupu mengine

No comments: