Wednesday, March 14, 2012

JUST IN: BOT WAONGHEZA MUDA WA KUREKEBISHA TAARIFA BENKI


BENKI Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa mwaka mmoja kwa wateja wa benki zote nchini kuboresha taarifa zao kuanzia kesho Machi 15, 2012 hadi Machi 14, 2013.

Benki na taasisi zote za fedha zimejulishwa kuzingatia kikamilifu agizo hili. Agizo la awali lilitamka kwamba muda wa kuboresha taarifa za wateja wa benki ungelimalizika leo.

Mwaka jana (2011) Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, alitoa kipindi cha muda wa mwaka mmoja kuanzia Machi 15, 2011 hadi Machi 14, 2012 kwa ajili ya zoezi hilo. Hii ilikuwa ni kuziwezesha benki zote kuzingatia kanuni zilizomo katika Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu.

Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tanzania inawataka wananchi na wateja wa benki nchini kutimiza wajibu wao kwa kujaza fomu za taarifa zao ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kushindwa kutimiza sharti hilo la kisheria.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano na Itifaki
BENKI KUU YA TANZANIA
Machi 14, 2012

No comments: