Thursday, March 15, 2012

Mama Salma Kikwete aongoza Matembezi ya Kuadhimisha siku ya Utepe Mweuope nchini

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete (mwenye traki suti) akipokea maelezo kutoka kwa Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii,Dkt. Hadji Mponda kabla ya kuanza matembezi ya kuadhimisha siku ya utepe mweupe Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mwenekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete (alievaa traki suti) pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na taasisi mbalimbali zinazoshughulikia mpango wa uzazi salama na afya za watoto wakishiriki kwenye matembezi ya kuadhimisha utepe mweupe nchini.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Sadick.
Matembezi yakiendelea.
wanafunzi wakiwa na mabango.
Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiongoza matembezi hayo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akikata utepe kuzindua kitabu cha uzazi salama leo jijini Dsm wakati wa maadhimisho ya suku ya utepe mweupe Tanzania.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Mecky Sadick.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akizindua kitabu cha okoa maisha.Kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Mecky Sadick na kushoto Mwenyekiti wa Uteme Mweupe nchini,Rose Mlay.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Rose Ntambuto wa taasisi ya Engender Health chini ya mradi wa ACQUIRE Tanzania leo jijini DSM kuhusu shughuli za taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya utepe mweupe Tanzania.
Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka banda la PSI.
Mjomba Mpoto akitumbuiza.
washiriki wa maandamano wakisikilia hotuba ya Mama Salma Kikwete.
wanachi wakiwa katika banda la PSI.
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

No comments: