Thursday, March 15, 2012

NYOSHI KUWAFUNDISHA MUSIC ACADEMY.
Kutoka kushoto Asha Baraka, Nyoshi, Mzee kalala na Nocha.
Wana Academy wakipewa somo kutoka kwa Nyoshi  (hayupo pichani).
Salam,
Raisi wa Bendi FM Academy na mkali wa masauti Nyoshi amejiunga  rasmi kwenye Music Academy ili kutoa fursa ya kuwafundisha wanafunzi namna ya kuimba vizuri vilevile kuwapatia uzoefu. Nyoshi ataungana na Mzee kalala pamoja na Mandela kutoka Twanga katika mjumuisho wa pamoja wa kutoa mafunzo halisi ya muziki ili kuwanoa ipasavyo wana academia na hatimaye kuweza kufanikiwa kuibua vipaji vya muziki nchini Tanzania.
Music Academy imejikita zaidi katika kutoa mafunzo na pia kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
Asanteni,Imeandaliwa na ASET Pamoja na URBAN PULSE CREATIVE.

No comments: