Saturday, April 7, 2012

Katibu Mkuu wa CCM ashiriki kumbukumbu za miaka 18 ya mauaji ya kimbali nchini Rwanda



Katibu Mkuu wa CCM ndugu Wilson C. Mukama na mkewe Mama Sophia Mukama, wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la pamoja la wahanga wa mauaji ya halaiki yaliyotokea Mwaka 1994 Kigali Rwanda. Mukama yupo nchini Rwanda kufuatia Mwaliko wa Katibu Mkuu wa RPF kushiriki katika kumbukumbu za miaka 18 ya mauaji ya kimbali.
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Wilson C. Mukama, akiongea na waandishi wa wa habari mara baada ya kutembelea makumbusho ya Kigali ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Mukama yupo nchini Rwanda kufuatia Mwaliko wa Katibu Mkuu wa RPF kushiriki katika kumbukumbu za miaka 18 ya mauaji ya kimbali.
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Wilson C. Mukama, akipewa maelezo na Katibu Mkuu wa RPF ( Chama Tawala cha Rwanda) ndugu Ngarambe Francois, ya namna mauaji ya halaiki ya Rwanda yalivyosababishwa na Wanasiasa wachochezi. Mukama alikuwa akitembelea Makumbusho ya Kigali ya mauaji ya halaiki yaliyotokea mwaka 1994.

No comments: