Monday, April 9, 2012

JE, NI NANI ANAYEMFARIJI MSICHANA HUYU WA MIAKA 18 ALIYEONDOKEWA NA MPENZI WAKE?




Ndugu zangu,
Ni kazi ngumu kuwa wakili kwa anayeonekana na jamii kuwa ni ‘ shetani’. Lakini, kwenye hili la kifo cha kusikitisha cha msanii Steven Kanumba kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwa bidii.
Kuna maswali pia ya kujiuliza juu ya msichana huyu wa miaka 18 ambaye sehemu kubwa ya jamii imeshamuhukumu kuwa ni muuaji.
Kuna hata ambao hawalijui jina lake la kamili, bali, anajulikana kama ‘ Lulu’.  Jina lake ni Elizabeth Michael .
Simulizi ya Lulu inaonyesha kuwa yeye na Kanumba walikuwa na mahusiano. Na wivu pia umeingia kwenye mahusiano yao. Hivyo basi, ugomvi na hatimaye kifo cha Kanumba.
Uchunguzi kamili haujakamilika. Na kama haujakamilika, basi, Lulu anabaki kuwa ni mtuhumiwa na si muhusika na kifo hicho. Kumwita Lulu muuaji  ni kuharakisha kutoa hukumu isiyo ya haki. Pamoja na machungu yetu, lakini wanadamu tunapaswa kuwa na subira.
Na ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani anayemfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?

4 comments:

Anonymous said...

Kwakweli, nadhani uchungu wake ni mkubwa zaidi, anahitaji faraja izingatiwe kuwa yeye ni mtuhumiwa ambaye jamii kubwa ishamuhukumu, mfiwa ambaye mapenzi wake kafariki katika ajali ambayo inasadikika yeye ndo kasababisha, Pole Elizabeth yakiisha badili Maisha yako.Barikiwa, Sali upate hukumu stahili.

Justine JBRugaimukamu said...

Inawezekana unatengeneza lugha ya 'kumsafisha' kabla taarifa ya uchunguzi haijatoka?.Ni kipi hakijulikani ktk maisha yakilasiku ya msichanahuyu binafsi,na maisha ya so called mastaa wa bongo?.Unadhani kilichotokea na historia halisi ya maishahayo kuna cha kushangaza?.Labda ni uono na uelewa wangu mdogo tu,nisamehewe kwa hilo.

Catherine steven said...

Elizabeth namshauri asikate tamaa zaidi azidi kumuomba mungu ampe faraja na nguvu ktk kipindi hki kigumu cha kupotelewa na mpenz wake.na akuna wakumpa faraja zaidi ya mungu wake.

emuthree said...

Ukweli na haki itafanya kazi yake, tuviachie vyombo vya dola...maana yanayoongewa sasa ni upande mmoja wa shilingi tu