Saturday, April 7, 2012

Kanumba: Nyota ya Tanzania iliyozimika mapemaNa Fredrick Bundala- Tone Radio-Tz

Usiku wa kuamkia Jumamosi ya Pasaka haitasahaulika kamwe kwa mashabiki wa filamu Tanzania. Asante kwa kukua haraka kwa mawasiliano ya simu na mitandao ya jamii kama Facebook na Twitter, habari zilianza kuenea haraka mithiri ya blue inavyoingia kwenye shati jeupe. Wengine waliokuwa wamezima simu zao ili kufurahia usingizi wao pasipo kusumbuliwa na jumbe ama miito ya usiku waliamka na kuzikuta habari kwa majirani, radioni ama baada ya meseji zilizokuwa ‘pending’ kuingia “Kanumba hatuko naye tena”. Nini????? Ni swali ambalo wengi waliliuliza kwa sauti ya kupaza kuashiria jinsi walivyoshtushwa na habari hiyo.
Katika dunia hii ya leo yenye kila aina ya mihangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku, si ajabu mpaka sasa kuna watu wengine hawana taarifa zozote. Kwa wote, waliopata habari hii mbaya mapema na wale waliochelewa kuipata, upokeaji wake ulikuwa sawa…Mshtuko mkubwa. Kuanzia asubuhi ya jumamosi April 7, 2012, mada iliyokuwa imetawala mitandao kijamii husasan Facebook na Twitter ilihusu kifo cha Kanumba. Navyo vituo vya radio na runinga vilibidi visitishe matangazo ya kawaida na kufanya vipindi maalum kwa kuwahoji watu wa karibu na Kanumba ili kuyajibu maswali mengi yanayovizunguka vichwa vya wananchi wengi wanaomfahamu.Mamia ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wameendelea kuelezea ni kiasi gani wameumizwa na kifo cha Kanumba, msanii wa filamu ambaye pasi na shaka ndiye aliyekuwa na mafanikio kuliko msanii yeyote katika tasnia hiyo iliyochupia kwa kasi.Kwa mujibu wa mdogo wake Chanzo cha kifo chake kinadaiwa kutokana na ugomvi kati yake na mpenzi wake ambaye ni muigizaji wa filamu Elizabeth ambaye ni maarufu kwa jila Lulu. Kwa wengi taarifa za kuwa kumbe! Kanumba na Lulu walikuwa wapenzi zimefahamika katika muda mbaya kabisa. Imedaiwa kuwa Lulu alikwenda nyumbani kwa Kanumba na baadaye kukazuka ugomvi. Vyanzo vingine vinadai kuwa ugomvi huo ulitokana na Kanumba kuchukizwa na mazungumzo ya simu aliyokuwa akiyafanya na mtu ambaye inadaiwa ni mwanaume. Wapenzi hao waliingia chumbani na baadaye Lulu kumfuata mdogo wake Kanumba aliyekuwa akiishi naye kumwambia kuwa Kanumba ameanguka. Alipoenda alimkuta kaanguka huku akitokwa na povu mdomoni na kuamua kumuita daktari wa Kanumba kisha kuchukua uamuzi wa kumpeleka hospitali Muhimbili ambako ndiko alikofariki dunia.Taarifa zingine zimedai kuwa Lulu alimsukuma Kanumba na kuangikia sakafuni. Hadi hivi sasa Lulu yupo katika kituo cha polisi OysterBay na bila shaka baada ya muda kutakuwepo na taarifa rasmi ya namna kifo chake kilivyotokea. Kumekuwa na taarifa pia kuwa Lulu amejeruhiwa pia usoni usoni kutokana na ugomvi huo.Imewawia vigumu wapenzi wa Kanumba kuzizuia hasira zao dhidi ya Lulu ambaye wanaamini ndiye chanzo cha kuondoka kwake duniani katika muda ambao bado wanamhitaji. Suala la kama Lulu amehusika moja kwa moja katika kifo chake linabaki kuwa mikononi mwa vyombo vya dola. Kifo chake kimewaumiza wengi kuanzia watu wa kawaida, wanasiasa, watu wenye nafasi kubwa kwenye makampuni nchini na wasanii wenzake.Mtoto wa kiume wa rais Jakaya Kikwete Ridhiwani Kikwete anasema “Steve, what a loss! Tumepoteza mtu wa kuigwa na nyota katika tasnia ya filamu inayochupikia na iliyoajiri maelfu ya vijana. Sala zangu ziende kwa familia ya Kanumba na kwa mamilioni ya mashabiki wake ndani na nje ya nchi, mimi nikiwa mmoja wao. Umekuwa muigizaji mkubwa zaidi katika kipindi chako nchini mwetu. Utakoswa na mamilioni. Umeondoka mapema mno”Mwamvita Makamba ambaye ni ofisa katika kampuni ya Vodacom anasema “Ingekuwa ngumu kutokitamani kipaji chake kikubwa” huku mwanamitindo Flaviana Matata akisema nimeamka na kukuta habari ya kusikitisha, pumzika pema Kanumba, rafiki na mtu wa nyumbani (Shinyanga). Ni huzuni. Maisha ni mafupi sana.Salamu nyingi za rambirambi zinaendelea kumiminika kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wa kulipwa wa kikapu katika ligi ya mchezo huo nchini Marekani, mbunge wa Bumbuli January Makamba, Zitto Kabwe, Nancy Sumari, kituo cha televisheni cha nchini Afrika kusini Channel O na wengine wengi.Hakuna asiyemfahamu Stephen Kanumba nchini Tanzania. Hata kwa wasio wapenzi wa filamu nchini, hawakuweza kuikwepa sura yake. Jina lake lilikuwa na litaendelea kutajwa na watu wa rika mbalimbali.Kwa watoto ambao tafiti zinaonesha kuwa ndio wapenzi wakubwa wa filamu za Tanzania, kifo kimemchukua shujaa wao. Walimwona Kanumba kama mfano halisi wa mtu aliyefanikiwa na wangependa wakiwa wakubwa waje kuwa waigizaji kama yeye.Watoto hawa na wapenzi wengine wa filamu nchini wamempoteza mtu aliyekuwa akibandika tabasamu katika sura zao kwa uigizaji wake mahiri katika filamu. Mwenyezi Mungu alimjalia kipaji cha uigizaji na akaanza kukikuza katika umri mdogo kwa kuigiza darasani. Uigizaji ni kitu kilichokuwa kwenye damu yake hivyo aliamua kujiunga na kundi la Kaole kwa ajili ya mafunzo ya uigizaji na pia kupokea mafunzo ya masuala hayo kutoka kwa Dr. Nyoni wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.Kipaji chake kilionekana katika tamthilia zilizotayarishwa na kurushwa katika kituo cha ITV ambazo miongoni mwake ni ‘Jahazi’, ‘Dira’, ‘Zizimo’, ‘Tufani’, ‘Sayari’, ‘Taswira’, ‘Ghariika’ na ‘Baragumu’
Ujio wake uliziongezea utamu tamthilia hizo zilizokuwa maarufa sana kuliko filamu. Mara nyingi aliigiza kama kijana maskini lakini aliyejaaliwa kipaji kikubwa cha kupambanua mambo na busara nyingi kiasi cha kuwa kipenzi cha akinadada wenye uwezo katika tamthilia hizo.Pamoja na kuwa maarufu katika tamthilia hizo, kipato alichokuwa akilipwa hakikuweza kwendana na umaarufu wake uliokuwa ukienea kwa kasi nchini.Aligundua kuwa kipaji chake kitamfikisha mbali kama akijiingiza kwenye uigizaji wa filamu na kutupa karata yake ya kwanza katika filamu iliyoitwa Haviliki. Tangu hapo milango ikaanza kufunguka mmoja baadaya mwingine. Kila filamu aliyokuwa akiitoa ilipendwa na wapenzi wa filamu na kumfanya kuwa muigizaji mwenye filamu zinazouzika zaidi nchini.Kuthubutu kwa Kanumba kulimpelekea kupata mafanikio makubwa si tu nchini bali katika bara zima la Afrika pamoja na kufanikiwa kuwa na kampuni yake mwenyewe ya filamu. Jitihada zake na za wasanii wengine wa filamu wenye hadhi yake, zimepelekea Tanzania kuwa nchi inayojulikana sana barani Afrika kwa filamu zake zinazopendwa na pia kuendelea kuikuza lugha ya Kiswahili.Hakuna aliyewahi kuwaza kuwa siku moja waigizaji wa Tanzania watakuja kuigiza pamoja na wale wa Nigeria ambao wao walianza kitambo. Dar to Lagos ilimfungulia mipaka barani Afrika na kuthibitisha kuwa yote yanawezekana. Kanumba alikuwa amefikia kuwa nyota wa Afrika nzima hasa baada ya kufanikiwa kuigiza katika filamu moja na Ramsey Noauh ambaye umaarufu wake katika filamu barani Africa hauna kifani. Devil Kingdom ilithibitisha kuwa sasa Kanumba amefika mbali na ni tishio kwa wasanii wa Afrika nzima. Inatia majonzi makubwa kwakuwa jumanne ya tarehe 3, april, 2012 kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa Devil Kingdom itaoneshwa katika jumba la sinema la Silverbird mjini Accra, Ghana. Hiyo ni ishara kuwa jina lake lilikuwa linaenea kwa kasi katika nchi zilizo mbali kijiographia na Tanzania.Amewahi kuonesha nia ya kupeleka kipaji chake Hollywood na kwa uthubutu aliouonesha, bila shaka angeweza kuifikia ndoto hiyo. Katika umri mdogo aliokuwa nao ameweza kufanya mambo makubwa kiasi ambacho wengi wanawaza ingekuaje kama mwenyenzi Mungu angemwacha aishi miaka thelathini zaidi. Kwa namna yoyote ile, mshumaa wa maisha ya Kanumba umezimika mapema mno. Hakuna atakayeliziba pengo lake. Tasnia ya Filamu nchini imepata pigo kubwa kulihimili. Tanzania imempoteza mpeperushaji muhimu wa bendera yake katika majukwaa ya kimataifa.Watoto ambao ni mashabiki wake wakubwa, watakua wakimkumbuka Kanumba. Mashabiki wake kwa ujumla watazikosa filamu zake zilizokuwa zikisubiriwa kila filamu mpya inaposambazwa. 
Ni msiba mkubwa sana nchini.Ni wazi kuwa mazishi yake yatahudhuriwa na wengi si kutoka Tanzania bali hata mashabiki wake wa Afrika mashariki watakaokuwa na uwezo wa kuja nchini. Ni muda ambao vyombo vya habari vya Tanzania vitakuwa katika ushindani mkubwa wa kuyatangaza mazishi yake kwa ufanisi. Kanumba amefariki katika muda ambao mafanikio yake yalikuwa yamegota kileleni hivyo si ajabu kwa wiki kadhaa akatawala mazungumzo ya mtaani, kazini na vibarazani. Roho yake ilale mahala pema peponi, Amen. Usiku wa kuamkia Jumamosi ya Pasaka haitasahaulika kamwe kwa mashabiki wa filamu Tanzania. Asante kwa kukua haraka kwa mawasiliano ya simu na mitandao ya jamii kama Facebook na Twitter, habari zilianza kuenea haraka mithiri ya blue inavyoingia kwenye shati jeupe. Wengine waliokuwa wamezima simu zao ili kufurahia usingizi wao pasi kusumbuliwa na jumbe ama miito ya usiku waliamka na kuzikuta habari kwa majirani, radioni ama baada ya meseji zilizokuwa ‘pending’ kuingia “Kanumba hatuko naye tena”. Nini????? Ni swali ambalo wengi waliliuliza kwa sauti ya kupaza kuashiria jinsi walivyoshtushwa na habari hiyo.
Katika dunia hii ya leo yenye kila aina ya mihangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku, si ajabu mpaka sasa kuna watu wengine hawana taarifa zozote. Kwa wote, waliopata habari hii mbaya mapema na wale waliochelewa kuipata, upokeaji wake ulikuwa sawa…Mshtuko mkubwa. Kuanzia asubuhi ya jumamosi April 7, 2012, mada iliyokuwa imetawala mitandao kijamii husasan Facebook na Twitter ilihusu kifo cha Kanumba. Navyo vituo vya radio na runinga vilibidi visitishe matangazo ya kawaida na kufanya vipindi maalum kwa kuwahoji watu wa karibu na Kanumba ili kuyajibu maswali mengi yanayovizunguka vichwa vya wananchi wengi wanaomfahamu.Mamia ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wameendelea kuelezea ni kiasi gani wameumizwa na kifo cha Kanumba, msanii wa filamu ambaye pasi na shaka ndiye aliyekuwa na mafanikio kuliko msanii yeyote katika tasnia hiyo iliyochupia kwa kasi.Kwa mujibu wa mdogo wake Chanzo cha kifo chake kinadaiwa kutokana na ugomvi kati yake na mpenzi wake ambaye ni muigizaji wa filamu Elizabeth ambaye ni maarufu kwa jila Lulu. Kwa wengi taarifa za kuwa kumbe! Kanumba na Lulu walikuwa wapenzi zimefahamika katika muda mbaya kabisa. Imedaiwa kuwa Lulu alikwenda nyumbani kwa Kanumba na baadaye kukazuka ugomvi. Vyanzo vingine vinadai kuwa ugomvi huo ulitokana na Kanumba kuchukizwa na mazungumzo ya simu aliyokuwa akiyafanya na mtu ambaye inadaiwa ni mwanaume. Wapenzi hao waliingia chumbani na baadaye Lulu kumfuata mdogo wake Kanumba aliyekuwa akiishi naye kumwambia kuwa Kanumba ameanguka. Alipoenda alimkuta kaanguka huku akitokwa na povu mdomoni na kuamua kumuita daktari wa Kanumba kisha kuchukua uamuzi wa kumpeleka hospitali Muhimbili ambako ndiko alikofariki dunia.Taarifa zingine zimedai kuwa Lulu alimsukuma Kanumba na kuangikia sakafuni. Hadi hivi sasa Lulu yupo katika kituo cha polisi OysterBay na bila shaka baada ya muda kutakuwepo na taarifa rasmi ya namna kifo chake kilivyotokea. Kumekuwa na taarifa pia kuwa Lulu amejeruhiwa pia usoni usoni kutokana na ugomvi huo.Imewawia vigumu wapenzi wa Kanumba kuzizuia hasira zao dhidi ya Lulu ambaye wanaamini ndiye chanzo cha kuondoka kwake duniani katika muda ambao bado wanamhitaji. Suala la kama Lulu amehusika moja kwa moja katika kifo chake linabaki kuwa mikononi mwa vyombo vya dola. Kifo chake kimewaumiza wengi kuanzia watu wa kawaida, wanasiasa, watu wenye nafasi kubwa kwenye makampuni nchini na wasanii wenzake.Mtoto wa kiume wa rais Jakaya Kikwete Ridhiwani Kikwete anasema “Steve, what a loss! Tumepoteza mtu wa kuigwa na nyota katika tasnia ya filamu inayochupikia na iliyoajiri maelfu ya vijana. Sala zangu ziende kwa familia ya Kanumba na kwa mamilioni ya mashabiki wake ndani na nje ya nchi, mimi nikiwa mmoja wao. Umekuwa muigizaji mkubwa zaidi katika kipindi chako nchini mwetu. Utakoswa na mamilioni. Umeondoka mapema mno”Mwamvita Makamba ambaye ni ofisa katika kampuni ya Vodacom anasema “Ingekuwa ngumu kutokitamani kipaji chake kikubwa” huku mwanamitindo Flaviana Matata akisema nimeamka na kukuta habari ya kusikitisha, pumzika pema Kanumba, rafiki na mtu wa nyumbani (Shinyanga). Ni huzuni. Maisha ni mafupi sana.Salamu nyingi za rambirambi zinaendelea kumiminika kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wa kulipwa wa kikapu katika ligi ya mchezo huo nchini Marekani, mbunge wa Bumbuli January Makamba, Zitto Kabwe, Nancy Sumari, kituo cha televisheni cha nchini Afrika kusini Channel O na wengine wengi.Hakuna asiyemfahamu Stephen Kanumba nchini Tanzania. Hata kwa wasio wapenzi wa filamu nchini, hawakuweza kuikwepa sura yake. Jina lake lilikuwa na litaendelea kutajwa na watu wa rika mbalimbali.Kwa watoto ambao tafiti zinaonesha kuwa ndio wapenzi wakubwa wa filamu za Tanzania, kifo kimemchukua shujaa wao. Walimwona Kanumba kama mfano halisi wa mtu aliyefanikiwa na wangependa wakiwa wakubwa waje kuwa waigizaji kama yeye.Watoto hawa na wapenzi wengine wa filamu nchini wamempoteza mtu aliyekuwa akibandika tabasamu katika sura zao kwa uigizaji wake mahiri katika filamu. Mwenyezi Mungu alimjalia kipaji cha uigizaji na akaanza kukikuza katika umri mdogo kwa kuigiza darasani. Uigizaji ni kitu kilichokuwa kwenye damu yake hivyo aliamua kujiunga na kundi la Kaole kwa ajili ya mafunzo ya uigizaji na pia kupokea mafunzo ya masuala hayo kutoka kwa Dr. Nyoni wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.Kipaji chake kilionekana katika tamthilia zilizotayarishwa na kurushwa katika kituo cha ITV ambazo miongoni mwake ni ‘Jahazi’, ‘Dira’, ‘Zizimo’, ‘Tufani’, ‘Sayari’, ‘Taswira’, ‘Ghariika’ na ‘Baragumu’
Ujio wake uliziongezea utamu tamthilia hizo zilizokuwa maarufa sana kuliko filamu. Mara nyingi aliigiza kama kijana maskini lakini aliyejaaliwa kipaji kikubwa cha kupambanua mambo na busara nyingi kiasi cha kuwa kipenzi cha akinadada wenye uwezo katika tamthilia hizo.Pamoja na kuwa maarufu katika tamthilia hizo, kipato alichokuwa akilipwa hakikuweza kwendana na umaarufu wake uliokuwa ukienea kwa kasi nchini.Aligundua kuwa kipaji chake kitamfikisha mbali kama akijiingiza kwenye uigizaji wa filamu na kutupa karata yake ya kwanza katika filamu iliyoitwa Haviliki. Tangu hapo milango ikaanza kufunguka mmoja baadaya mwingine. Kila filamu aliyokuwa akiitoa ilipendwa na wapenzi wa filamu na kumfanya kuwa muigizaji mwenye filamu zinazouzika zaidi nchini.Kuthubutu kwa Kanumba kulimpelekea kupata mafanikio makubwa si tu nchini bali katika bara zima la Afrika pamoja na kufanikiwa kuwa na kampuni yake mwenyewe ya filamu. Jitihada zake na za wasanii wengine wa filamu wenye hadhi yake, zimepelekea Tanzania kuwa nchi inayojulikana sana barani Afrika kwa filamu zake zinazopendwa na pia kuendelea kuikuza lugha ya Kiswahili.Hakuna aliyewahi kuwaza kuwa siku moja waigizaji wa Tanzania watakuja kuigiza pamoja na wale wa Nigeria ambao wao walianza kitambo. Dar to Lagos ilimfungulia mipaka barani Afrika na kuthibitisha kuwa yote yanawezekana. Kanumba alikuwa amefikia kuwa nyota wa Afrika nzima hasa baada ya kufanikiwa kuigiza katika filamu moja na Ramsey Noauh ambaye umaarufu wake katika filamu barani Africa hauna kifani. Devil Kingdom ilithibitisha kuwa sasa Kanumba amefika mbali na ni tishio kwa wasanii wa Afrika nzima. Inatia majonzi makubwa kwakuwa jumanne ya tarehe 3, april, 2012 kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa Devil Kingdom itaoneshwa katika jumba la sinema la Silverbird mjini Accra, Ghana. Hiyo ni ishara kuwa jina lake lilikuwa linaenea kwa kasi katika nchi zilizo mbali kijiographia na Tanzania.Amewahi kuonesha nia ya kupeleka kipaji chake Hollywood na kwa uthubutu aliouonesha, bila shaka angeweza kuifikia ndoto hiyo. Katika umri mdogo aliokuwa nao ameweza kufanya mambo makubwa kiasi ambacho wengi wanawaza ingekuaje kama mwenyenzi Mungu angemwacha aishi miaka thelathini zaidi. Kwa namna yoyote ile, mshumaa wa maisha ya Kanumba umezimika mapema mno. Hakuna atakayeliziba pengo lake. Tasnia ya Filamu nchini imepata pigo kubwa kulihimili. Tanzania imempoteza mpeperushaji muhimu wa bendera yake katika majukwaa ya kimataifa.Watoto ambao ni mashabiki wake wakubwa, watakua wakimkumbuka Kanumba. Mashabiki wake kwa ujumla watazikosa filamu zake zilizokuwa zikisubiriwa kila filamu mpya inaposambazwa. 
Ni msiba mkubwa sana nchini.Ni wazi kuwa mazishi yake yatahudhuriwa na wengi si kutoka Tanzania bali hata mashabiki wake wa Afrika mashariki watakaokuwa na uwezo wa kuja nchini. Ni muda ambao vyombo vya habari vya Tanzania vitakuwa katika ushindani mkubwa wa kuyatangaza mazishi yake kwa ufanisi. Kanumba amefariki katika muda ambao mafanikio yake yalikuwa yamegota kileleni hivyo si ajabu kwa wiki kadhaa akatawala mazungumzo ya mtaani, kazini na vibarazani. Roho yake ilale mahala pema peponi, Amen.

No comments: