Leo ni siku ya Sheikh Abeid Aman Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar ambaye siku ya Ijumaa ya Aprili 7, mwaka 1972, aliuawa kwa kupigwa risasi wakati akicheza Dhumna yeye na maswahiba wake wa karibu katika makao makuu ya chama cha Afro Shirazi Kisiwandui, Unguja, ambayo sasa ni Makao Makuu ya CCM, Zanzibar.
Leo ni siku ya mapumziko na viongozi wa juu serikalini pamoja na wananchi wa visiwani wanakutanika hapo Kisiwandui kuzuru kaburi la Hayati Karume ambaye alizikwa hapo hapo makao makuu ya chama.
No comments:
Post a Comment