Friday, April 13, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA MPYA IKULU LEO

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo
 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwapongeza wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, na Makamu wake wawili, Maalim Seif na Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi wateule na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi. Tume hiyo inatarajia kuanza kazi rasmi Mei 01, mwaka huu. 


Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwantum Malale,  kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments: