Friday, April 13, 2012

RAUNDI YA 23 YA LIGI KUU YA VODACOM, POLISI DODOMA KUKIPIGA NA AZAM KESHO

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho inaingia raundi ya 23, ambapo itachezwa jumla ya mechi nne.
Polisi Dodoma wataikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjiniDodoma wakati JKT Ruvu watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Turiani.
Mechi nyingineza raundi hiyo zitakuwa kati ya Kagera Sugar na African Lyon zitakazooneshanakazi kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Nayo Moro United inaikaribishaOljoro JKT katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Raundi ya 23itakamilika Jumapili (Aprili 15 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ruvu Shooting naSimba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Yanga itakuwa mgeniwa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Villa Squaditapambana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Ligi hiyoitaendelea tena Aprili 18 mwaka huu kwa mechi tano. Kagera Sugar vs Yanga mjiniBukoba, Toto Africans vs African Lyon jijini Mwanza, JKT Ruvu vs Simba- Uwanjawa Taifa, Dar es Salaam, Ruvu Shooting vs Moro United mjini Mlandizi na PolisiDodoma vs Coastal Union mjini Dodoma.

No comments: