Sunday, April 8, 2012

SERIKALI ZA AFRIKA ZAOMBWA KUJIFUNZA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA



Balozi mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (kushoto) akisalimiana na Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga.Katikati ni Afisa habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Bw. Danford Mpumilwa.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akimkaribisha ukumbini Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga wakati  sherehe za maadhimisho ya miaka 18 ya Kimbari leo jijini Dar es Salaam.
Balozi mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert akizungumza kwa niaba ya serikali ya Rwanda  kuhusu maadhimisho ya mauaji ya Kimbari na kushukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wanaoutoa kwa nchi yake baada ya mauaji ya hayo ya mwaka 1994.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba rasmi ya kuadhimisha Mauaji ya Kimbari na kuwahakikishia Wanyarwanda kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Rwanda.
Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga akitoa hotuba yake ya Maendeleo ya Kesi za mauaji ya Kimbari nchini Rwanda katika maadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam. Bw. Roland alisema kati ya kesi 92 za mauaji ya Kimbari 83 zimeshasikilzwa.
Mkurugenzi Mwakilishi wa shirika la kazi Duniani (ILO) Bw. Alexio Musindo akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari Rwanda leo jijini Dar es Salaam.
Afisa habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Bw. Danford Mpumilwa akimuonesha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim mabango mbalimbali ya kukumbuka mauaji ya Kimbari ya Rwanda wakati maadhimisho ya miaka 18 ya Kimbari jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakisoma mabango na machapisho mbalimbali ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda.
Tukio la kuwasha mishumaa kuwakumbuka waathirika wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994.
Mabalozi na wawakilishi mbalimbali wa Umoja  wa Mataifa wakifuatilia hotuba ya Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Mh. Zitto Kabwe (wa kwanza kushoto) alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

No comments: