Friday, April 20, 2012

WAZIRI WA NISHATI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA.

Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Matiafa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini kwake jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo vikao vya Bunge vinaendelea.
Mh. Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasili kutoka katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusu Nishati uliofanyika nchini Ubelgiji. 
Mh. Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishati ambapo Umoja wa Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka 2030.
Mh. Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswa upatikanaji wa fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchini Tanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwa jitihada zake kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu ni haki ya msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upewe umakini mkubwa.
Pia ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa ni pamoja na kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.
Kusoma zaidi: http://tz.one.un.org
Imetolewa na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa – Afisa Mawasiliano.


No comments: