Wednesday, October 12, 2011

BASI LA SHABCO EXPRESS LAPATA AJALI MBAYA ENEO LA MSAMBIAZI, KOROGWE

Basi la Shabco Express ambalo lilikuwa likieleka Arusha leo limepata ajalimbaya ya kupinduka katika kona za Msambizi, Korogwe. Kwa mujibu wa abiria haowalisema kuwa gari hilolilipata ajali hiyo baada ya kulikwepa gari dogo na kujikuta likitumbukia mtalonikutoka na hali ya mvua na ukungu uliokuwa umeenea barabara nzima. Hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo
Abiria wakiwa wanaangalia ustarabu wa kusubiri gari lingine ili waendelee na safari yao, hapo ilikuwa ni majira ya saa tisa mchana huku mvua ikinyesha.
Abiria wakinyeshewa huku wakiwa na watoto wadogo mgongoni.
Gari hilo likionekana kwa upande wa nyuma.
Picha zote kwa Hisani ya Habari na Matukio Blog

No comments: