Wednesday, October 12, 2011

Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanazania Bara kwa upande wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yaendelea kijijini Butiama

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kuhusu Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Afisa Vijana, Bw. Florens Karist wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa upande wa Wizara hiyo yanayoendelea Kijijini Butiama Mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akielezea jambo wakati alipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (katikati) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara nyumbani kwake Butiama Mkoani Mara. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanazania Bara kwa upande wa Wizara hii zinazoendelea Katika viwanja vya Joseph Kazurira Nyerere kijijini Butiama. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu, Bi. Sihaba Nkinga na kulia kwake ni Diwani wa Kata ya Butiama Mhe. Peter Wanzagi.

No comments: