Tuesday, October 11, 2011

MUUMINI WA KANISA LA LAST CHURCH AFANYA MAOMBI, AGOMA KUMZIKA MWANAE KWA SIKU MBILI, ADAI ATAMFUFUA KAMA LAZARO

Wananchi waliofika kuomboleza msibani katika mtaa wa Mwaka kati mji mdogo wa Tunduma lakini Baba wa Marehemu Bwana Asanwisye Mwampamba aliamua kuwatimua kwa madai mwanae Bi Rhoida Mwampamba hajafa.

Muumini wa kanila la Last Church lililopo mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya leo amewazuia wakazi wa mtaa wa Mwaka kati Mwaka kulia katika msiba wa motto wake na kuzuia taratibu zote za mazishi kwa kile alichodai mwanawe hajafa amelala.

Bwana Asanwisye Mwampamba mwenye umri wa miaka 72 alipata taarifa za kufariki mwanawe Rhoida Mwampamba mwenye umri wa miaka 35, mama mwenye watoto wawili wa kike na wa kiume kutoka kwa binti yake aitwaye Sarah Mwampamba mwenye umri wa miaka 18 kwamba dada yake amefariki majira ya saa 8 kamili usiku wa kuamkia jana.

Lakini tangu muda huo alianza maombi kuwa mwanawe amelala hivyo hakuna sababu ya watu kulia na kutanga msiba.

Kwa upande wake mtendaji wa kitongoji cha Mwaka kati Bwana Godnes Mwaipula alipoitwa katika tukio hilo alifika lakini mzee huyo aliendelea na maombi akiamini kuwa mwanae amelala, ndipo mtendaji huo alipochukua jukumu la kwenda kumwita Mwenyekiti wa mji mdogo wa Tunduma Bwana Elias Cheyo.

Hata hivyo mwenyekiti Bwana Cheyo alifika katika eneo la maombi ambapo alishiriki kumwombea Bi Rhoida na ndipo kadri masaa yanavyozidi kuyoyoma hadi kufikia saa 12 kamili asubuhi, akachoka na hivyo akamshauri mzee huyo kuamini kuwa mwanae amefariki ambapo mzee huyo aliendelea na msimamo wakuwa mwanae amelala.

Kwa upande wake Mwenyekiti Bwana Cheyo amesema kuwa majira ya saa 7 mchana serikali iliamua kuingilia kati na kuuzika mwili wa marehemu huyo.

No comments: